August 28, 2016Kocha wa zamani wa Yanga, Tom Saintfiet amebarikiwa kupata mtoto, binti baada ya mkewe kujifungua juzi.

Saintfiet aliyewahi kuinoa Yanga na kuibebesha Kombe la Kagame, ameonyesha furaha kubwa kwa kutundika picha mtandaoni akielezea ujio wa mgeni huyo muhimu kwenye familia yake.

Kocha huyo Mbelgiji, aliwahi kuinoa Yanga, pia Saint George ya Ethiopia. Pia aliwahi kuwa kocha wa timu ya taifa ya Togo ambayo nahodha wake ni Emmanuel Adebayor.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV