August 9, 2016

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amekumbana na mashabiki wa Yanga wanaompinga kuhusiana na yeye kuzungumzia mkataba wao wa kukubali Mwenyekiti wao Yusuf Manji kupitia kampuni, kuwekeza kwa miaka kumi.

Makonda amtupia kwenye mtandao wa kijamii na kusema” Unataka kujua kwa nini Tanzania ni masikini pamoja na utajiri mkubwa wa maliasili tulizonazo? Soma mkataba wa Yanga wanaosaini leo”.

Kitendo hicho kimeonyesha kuwadhi baadhi ya mashabiki wa Yanga ambao walianza ‘kumshambulia’ kwa maneno, wengine wakimtaka kuzungumzia Simba na si Yanga.

Baadhi walimkumbusha mikataba kadhaa serikalini kama ile ya madini.

Inaonekana wazi, mashabiki hao hawakutana kuijadili kauli ya Makonda kwa kuwa alikuwa mgeni rasmi katika tamasha la Simba Day akionekana amevaa jezi ya Simba kwenye Uwanja wa Taifa, jana.1 COMMENTS:

  1. mchezo huu hauhitaji hasira....pole ndala kwa kujifanya mnajua kumbe hamna lolote

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV