August 22, 2016

Kiungo wa zamani wa Arsenal, Patrick Vieira amesema hofu yake ni kuwa timu yake hiyo ya zamani inaweza kuendelea kukosa ubingwa kama hakutakuwa na mabadiliko ya kiuchezaji hasa kutokana na kukosa aina ya wachezaji wenye sifa ya kutaka ubingwa na wenye nguvu ya kupambana kama ilivyokuwa enzi zao.

     
Wenger


Wachezaji wa Arsenal wa sasa

Vieira enzi zake alipokuwa Arsenal

Mkongwe huyo ambaye alikuwemo katika kikosi cha Arsenal ambacho kilicheza mechi 49 bila kufungwa kikijulikana kwa jina la ‘The Invincibles’ amesema Arsenal inayonolewa na Arsene Wenger inacheza soka zuri lakini haina wachezaji wenye nguvu ya kupambana dhidi ya wapinzani imara.


 
“Katika kizazi chetu tulikuwa na wachezaji wenye uwezo mkubwa na wengi wao walikuwa na nguvu kimwili.

“Tulikuwa na Dennis Bergkamp aliyekuwa anaweza kufunga, Thierry Henry ambaye alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya mengi, wengine ni kama kina Sol Campbell, Jens Lehmann, David Seaman wote walikuwa ni watu wenye nguvu na moyo wa kupambana.

“Kikosi chetu hicho kilikuwa kama ilivyokuwa ile Ufaransa Kombe la Dunia 1998.

“Nikiitazama Arsenal ya sasa nafurahia soka wanalocheza, wanacheza soka zuri katika ligi, lakini hofu yangu ni kuwa kuna vitu wanakosa kama vile nguvu na moyo au wa upambanaji.

“Kwa miaka mitano au sita iliyopita Arsenal imecjheza soka zuri la kisayansi na imesajili wachezaji wa aina hiyom wakiendelea hivyo watakuwa wanaonyesha uwezo na kuwemo katika mbio za ubingwa lakini mwisho wake wanakosa,” alisema Vieira ambaye sasa ni kocha wa New York City FC ya Marekani.

Vieira alivyo sasa

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic