August 22, 2016


Na Saleh Ally, Madrid
Awali nilitaka kubadili upepo kwenda Italia kwa ajili ya mechi ya Serie A kati ya AC Milan dhidi ya Torino baada ya kupata mwaliko wa Gianluca Zambrota, gwiji wa zamani wa AC Milan.

Lakini mwisho kutokana na usumbufu wa ubadishaji wa tiketi, nikaamua kubaki Hispania. Nisafiri kutoka Barcelona hadi Madrid, safari ya saa tatu kwa treni ya mwendo kasi kwelikweli.

Lengo lilikuwa ni kuona mechi yangu ya mwisho hapa wenyeji Atletico Madrid  dhidi ya Alaves ambayo imepanda daraja na timu ndogo. Ngoma ilikuwa inapigwa kwenye Uwanja wa Vicente Calderon jijini hapa.

Niliendelea kujifunza nje ya uwanja, namna ambavyo watu wanaungana kwa pamoja na kusherekea.

Timu mwenyeji kuwa na mashabiki asilimia 95, lakini pia utaona utamaduni ulivyo. Unapokwenda uwanjani, ni kuvaa jezi ili kuonyesha sapoti.


Ilikuwa ni raha sana hadi tunaingia uwanjani na mashabiki wengi waliamini timu yao mwenyeji ingeanza kwa kutoa kipigo dhidi ya wageni Alaves.

Kipindi cha kwanza, walishambulia kama mara nne, lakini ilikuwa hatari. Walishambuliwa sana lakini walikuwa bora kwenye ulinzi.

Dieogo Simeone aliona mambo si mazuri wakati wa mapumziko, aliamua kumuingiza Fernando Torres ambaye kweli aliongeza nguvu ikiwemo shuti lake kupiga mwamba baada ya kuwachambua mabeki wawili.

Pia ndiye alisababisha penalti dakika moja kabla ya mpira kwisha, walipofunga Alaves nao wakamwaga mboga dakika ya mwisho ya muwa wa nyongeza.

Mashabiki wa Atletico Madrid waliendelea kupiga makofi wakionyesha kuwakubali wachezaji wao kwa kuwa walionyesha juhudi. Lakini utaona hata wale mashabiki wa Alaves waliokuwa kidogo walijitahidi sana kuipongeza timu yao.

Hakukuwa na vurugu, utokaji uwanjani ulionyesha ni kundi la watu waliofika uwanjani kufurahia na si vurugu. Hakuna matusi wala watu kutaka kujulikana sana kwa kusema maneno ya kashfa.
Baada ya darasa jingine, leo naondoka tena kurejea Barcelona, kumalizia ziara yangu ya La Liga na Jumamosi nitakuwa na toleo maalum la mambo kadhaa niliyokusanya huku, nitatupia hapa, pia kwenye gazeti la Championi.





0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic