August 21, 2016


Benchi la ufundi la Simba limetoa siku moja tu ya mapumziko kwa kikosi chake baada ya kufanya kazi nzuri ya kuitwanga Ndanda FC kwa mabao 3-1 katika mechi ya ufunguzi wa Ligi Kuu Bara.

Hata hivyo, Simba wanatakiwa kurejea kazini kesho, kuendelea na maandalizi ya mechi nyingine zijazo.

Msemaji wa Simba, Haji Manara ameiambia SALEHJEMBE jijini Dar es Salaam, kwamba mazoezi yataendelea kesgo.

“Watarudi kazini kesho tayari kuendelea na maandalizi ya mechi nyingine, tayari mwamuzi amezungumza na wachezaji na kuwaeleza,” alisema Manara.


Simba imeanza ligi kwa kasi tofauti na misimu miwili mingine iliyopita ambayo kikosi hicho kilionekana zaidi kuanza kwa kusuasua.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV