August 21, 2016

Kufuatia kuwepo kwa tetesi nyingi juu ya uhusiano wake na mzazi mwenzake, Zari, staa wa wimbo wa Kidogo, Diamond Platnumz ameamua kutoa ya moyoni kuhusu mzazi mwenza huyo ambaye ni raia wa Uganda.  

Diamond ambaye amekuwa akizungumzwa mara kadhaa kuwa yupo katika mgogoro na mwandani wake huyo huku kukuwa na taarifa kuwa Zari ni mjamzito jambo ambalo wahusika walikuwa wagumu kulizungumza hadharani, sasa Diamond ameamua kuweka wazi kuwa Zari ni mjamzito.

Kauli hiyo ya Diamond ni kama inamaanisha kuwa amechoshwa na mambo au taarifa zinazoenea juu yake na Zari, huku pia ikidaiwa amerejesha ‘majeshi’ kwa mpenzi wake wa zamani Wema Sepetu kama ambavyo imekuwa ikidaiwa, lakini sasa ameamua kuweka wazi kila kitu.

Diamond na Zari

Baada ya kuandika kauli yake hiyo, kumekuwa na maoni mengi yanayoensdelea katika kurasa zake kijamii za msanii huyo aliyeanza kutamba kupita wimbo wa Mbagala.

  Kupitia kurasa zake za kijamii, Diamond ameandika haya:
“Ukiwa na Mwanamke Mzuri, Superstar, Ambae shilingi Mia miambili haimpigi chenga, Halaf ana akili, Akakuzalia Mtoto wa kike, Halaf mtoto nae Star, halaf akawa na Mimba yako Nyingine ya mtoto wakiume.. basi unajionea Mashia Muruaaaaaaaaaaaaaaaa...Lol yani Hapa najikuta kama sjui Biligeti Mzee wa Kwio Mi nampenda huyu dada Mwe @zarithebosslady”


Alichoandika Diamond


Kwa kauli hiyo sasa inamaanisha Diamond anatarajiwa kuitwa baba kwa mara ya pili kutoka kwa Zari ambaye ni mama Latiffa, mtoto wao wa kwanza ambaye alitimiza umri wa mwaka mmoja hivi karibuni.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic