August 24, 2016

Kufuatia Mtanzania, Alphonce Simbu kumaliza katika nafasi ya tano kwenye mbio za marathoni kwenye mashindano ya Olimpiki huko Rio De Janeiro, Brazil, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amempongeza kijana huyo na kuwashawishi Watanzania angalau kuridhika na mafanikio hayo madogo.

Simbu alikuwa mshindi wa tano akiwa amekimbia kwa saa 2:11.15 kwa tofauti ya dakika 2:17 nyuma ya mshindi wa kwanza, Eliud Kipchonge wa Kenya, katika mbio hizo zilizokuwa za umbali wa kilomita 42.

  


Akizungumza kuhusiana na hilo, Nape aliwataka Watanzania kuacha tabia ya kuwakatisha tamaa washiriki na badala yake kuwapongeza kwa haya mafanikio madogo wanayoyapata katika mashindano hayo, akitolea mfano wa Simbu kuvunja rekodi iliyodumu kwa takribani miaka 30 kwa Mtanzania kushika nafasi ya juu kwenye mbio kama hizo.

“Sawa kumekuwa na changamoto mbalimbali kwa washiriki wetu lakini wamejitahidi na Mtanzania mwenzetu akamaliza kwenye nafasi ya tano kwa kuvunja rekodi ya Suleiman Nyambui aliyemaliza katika nafasi ya sita miaka 30 iliyopita, sasa basi tumpongeze hata kwa hatua hii tuliyofikia leo.

“Tunafahamu wote kwamba bado tupo nyuma katika sehemu nyingi za michezo lakini pale ambapo tunaonyesha mwanga, wadau na Watanzania wote tuunge mkono na kuwatia moyo wanamichezo wetu, tusipende kulenga kukosoa sana, tuwe na utamaduni wa pongezi pia panapostahili,” alisema Nape.



SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic