November 4, 2018


Na George Mganga

Dakika 90 zimemalizika kutoka Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam kwa mabingwa wa kihistoria Yanga kulazimishwa suluhu ya bao 1-1 na Ndanda FC.

Yanga walikuwa wa kwanza kufungwa na Ndanda kupitia Nassor Hashim mnamo dakika ya 16 tu ya mchezo.

Yanga nao walifanikiwa kujibu mapigo kwa kusawazisha kupitia mpira wa adhabu ulipigwa na Ibrahim Ajibu ambao ulimfika Japhary Mohammed na kuumalizia kwa njia ya kichwa ikiwa ni dakika ya 24.

Matokeo hayo yanaifanya Yanga kufikisha alama 26 sawa na Simba ikiwa imecheza michezo 10.

Mpaka dakika 90 zinamalizika, Yanga 1-1 Ndanda FC.

8 COMMENTS:

  1. Kumradhi George kusema kwamba wamevutwa shati ni lugha rahisi pendelevu..sahihu ni wameponea chupuchupu pamoja na kubebwa na refa..Anyway karibuni nje ya Dar sasa ni mwendo wa sare au kufungw!Hero Simba waliopata safe kule...nyie hapo kwenu!

    ReplyDelete
  2. Lugha sahihi ni wamenusurika....sio kuvutwa shati.wangeshinda hapo kwa goli mmoja mgeandika kichwa kama wamefanya maajabu...saleh jembe mnazingua

    ReplyDelete
  3. Kwenye point hapo pako sahihi kweli!?

    ReplyDelete
  4. Kama Yanga wangetangulia kufunga hakafu Ndanda akarudishwa wangekuwa Yanga wamevutwa start..Lakini kwa kuwa Yanga wao ndio wamerudisha basis wamenusurika!

    ReplyDelete
  5. Salehe haya sasa unakuwaga na paltaza nyiingi kwa Makambo na Ajib kuliko hata Deo anaypangua mashuti ,na kocha alikuwa anapoonda wenziwe wanaofunga goli nyingi sasa hana hata akiba ya maneno na akina nani wale wa Azam akina KAIJAGE wanaosifia assist leo woote battery low

    ReplyDelete
  6. Kama hamuungani na kufanya uchaguzi na usajili wachezaji wenye ubora na kulisuka benchi la ufundi na idara ya utabibu na kufanya maandalizi ya kisayansi na kiuweledi kama Simba ubingwa msahau AZAM ANACHUKUA UBINGWA MARK MY WORDS!

    ReplyDelete
  7. Mikia FC ni povu tu! Yanga haijapoteza hii ni sare tu !

    ReplyDelete
    Replies
    1. This comment has been removed by the author.

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic