November 19, 2019


Taarifa zilizoenea zinaeleza kuwa baada ya Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems kuondoka kuelekea kwao Ubelgiji, kuna uwezekano klabu hiyo ikaachana naye.

Aussems aliondoka nchini jana kuelekea kwao ikielezwa sababu ni matatizo ya kifamilia lakini taarifa za ndani zinasema anaweza akafutwa kazi.

Inatajwa kuwa kuondolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika mapema dhidi ya UD Songo katika hatua ya awali ndicho kinachomhukumu Aussems ndani ya Simba.

Mbali na hilo, mwenendo wa kikosi hicho licha ya kuwa na matokeo mazuri katika ligi, namna kikosi kinavyocheza hakiwafurahishi wadau wengi wa Simba pamoja na mashabiki jambo ambalo linaelezwa linaweza sababisha kibarua chake kuota mbawa.

Leo hii kikosi hicho chini ya Msaidizi wake Denis Kitambi kitakuwa na mchezo wa kirafiki majira ya saa mbili za usiku dhidi ya JKT Tanzania, mechi ikichezwa Azam Complex.

10 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Gaspery Dastan,tulia sindano ikuingie kama hutaki basi nenda kasome blog zingine hii tuachie sisi kwa maana huyu Saleh ni mwanachama hai wa Mikia Fc hivyo hawezi kuichimba timu yake.

      Delete
    2. Yani mategemeo yako kocha Simba afukuzwe alafu we ndo uwe na furaha mi nilijua labda matatizo ya kwenye klabu yenu ya chura fc mshayamaliza kumbe kipele kinakuwasha kuifuatilia timu yenye malengo tofauti kabisa na nyie kandambili umechelewa sana si hata tukimfukuza kocha tuna sababu za msingi kulingana na malengo tuliyomuwekea tulimvumilia tu haya nyie mmefukuza Zahera mna sababu gani ya msingi

      Delete
    3. Hata Yanga ilimfukuza Zahera kwa sababu za msingi na mstakabali wa timu kwa ujumla. Kwan unadhan ninyi peke yenu mnamalengo? Na sifa ya malengo lazima yatofautiane kulingana na wadau husika

      Delete
  2. Tujue pia na kupongeza. sijawahi au ni mara chache sana tunapongeza. Tusitishie kutokusoma wakati tunafaidi sana humu. kama utaki kufuatilia si uondoke kimya kimya?. Kama kuna mapungufu wakati mwingine ni ya kibinadamu. Mwenzetu kathubutu kuanzisha.Sisi hatujathubutu. Mh!

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻🏃🏻

    ReplyDelete
  4. NA ASEPE TU TU ANATUZINGUA HADI LEO HANA FIRST ELEVEN YA KUSOMEAKA KILA SIKU ANAJARIBU WATU. AAAGH

    ReplyDelete
  5. Kuna fitina inafanyika hapo ili timu yetu ifanye vibaya

    ReplyDelete
  6. Kocha akishafundisha ni kazi ya wachezaji au naye anaingia uwanjani? Mbona Arsenal, Man City zinafungwa na kufanya vibaya? Mchezo wa soka una bahati pia ndani yake, huwezi kushinda wewe kila siku hata wenzetu wanapania kushinda vilevile.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic