September 5, 2016Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa amesema ataandika ripoti na kuiwasilisha TFF mara baada ya kumaliza mechi ya kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika.

Taifa Stars imemalizia mechi yake ya mwisho kuwania kucheza michuano hiyo baada ya kufungwa bao 1-0 na Nigeria.

“Kweli nitaifanyia kazi ripoti, nitaandika na kuiwasilisha kwa wahusika. Ndani yake kutakuwa na mambo mengi.

“Kikubwa ni kuangalia ni njia ipi ni sahihi, nini kilipungua na mapendekezo ya kuongeza kwa michuano ijayo,” alisema Mkwasa.

Katika mechi zake zote, Stars ilishinda mechi moja ikiwa ugenini dhidi ya Chad, lakini timu hiyo ikajitoa na kusababisha kuyeyusha matumaini ya Taifa Stars kabisa.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV