September 5, 2016

NDANDA FC

Kaimu Katibu Mkuu wa Ndanda FC, Selemani Kachere ametamba Jumatano wataamka katika mechi dhidi ya Yanga, Jumatano.

Kachere amesema wana imani kubwa wataanza kuinua matumaini ya kikosi chao kwa kuifunga Yanga.

“Tuna imani kubwa na kikosi chetu ingawa hatujaanza vizuri ligi. Hakika ligi ni ngumu na Yanga tunajua wana timu bora.

“Msimu uliopita na mwingine, Yanga walitufunga mara moja na sisi pia tumewafunga. Safari nyingine ilikuwa ni sare.

“Hivyo wajue wanakuja huku kumalizwa na wajiandae kuacha pointi tatu hapa Nangwanda Sijaona,” alisisitiza bosi huyo wa Ndanda.

Hiyo itakuwa ni mechi ya pili ya Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu huu, baada ya kuwa imeanza kwa kasi kwa kuichapa African Lyon kwa mabao 3-0.0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV