September 27, 2016Kikosi cha Fanja kimeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al Suwaiq katika Ligi Kuu ya Oman bila ya kuwa na washambuliaji wake wapya, Mrisho Ngassa na Danny Lyanga.

Fanya imeitwanga Al Suwaiq ambayo ilionekana kuwa kipi ngumu na hata kabla ya mechi, wachambuzi waliamini Fanja ambayo ni kongwe inaweza kupoteza.

Bila ya Ngassa wala Lyanga, Fanya imeibuka na ushindi huo kwenye Uwanja maarufu wa Seeb jijini Muscat.

Huenda wawili hao watalazimika kufanya maandalizi ya kutosha ikiwa ni pamoja na kumshawishi kocha kwamba wana uwezo na wapewe nafasi.


Ngassa amesajiliwa na Fanja baada ya kuvunja mkataba wake na Free State ya Afrika Kusini, huku Lyanga akitokea Simba na kujiunga na timu hiyo kongwe nchini Oman,

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV