September 21, 2016



Baada ya kuidungua Azam FC na kuipa timu yake ya Simba ushindi wa bao 1-0, kiungo mshambuliaji Shiza Kichuya ameweka hadharani kwamba nia yake ni kuona anaendelea kucheka na nyavu zaidi kwa ajili ya kuweka rekodi mbili kwenye timu hiyo kwa msimu huu.

Kichuya anayetumia vyema mguu wa kushoto amezitaja rekodi ambazo anataka kuandika kwenye timu hiyo ni kutwaa ufungaji bora ambao unashikiliwa na nyota wa Yanga, Amissi Tambwe pia kuipa ubingwa klabu hiyo baada ya kusota kwa miaka minne bila ya kombe lolote.

Kiungo huyo aliyetokea Mtibwa Sugar ya Morogoro asema kwamba ataendelea kuweka kambani mabao mengi zaidi kwa ajili ya kufanikisha azma zake za kuwa mfungaji bora sambamba na kuipa ubingwa timu yake.

 “Kufunga kwangu ni kawaida na nitahakikisha jambo hilo linaendelea kila nitakapopata nafasi kwa sababu nataka kuona ndoto zangu kwa msimu huu zikitimia kwa kufunga zaidi na kuwa mfungaji bora kama nitafanikiwa lakini kuipa ubingwa klabu yangu.

“Naamini hayo yatafanikiwa kama nitaendelea kuwa kwenye ubora wa sasa na naomba nisipate majeraha na kama nikifanikiwa juu ya hayo basi itakuwa ni mwendo wa mabao tu kama ambavyo imekuwa sasa,” alisema Kichuya. 


Tambwe anashikilia tuzo hiyo ya ufungaji bora kutokana na kuitwaa msimu uliopita mara baada ya kupachika kambani mabao 21 akifuatiwa na Hamis Kiiza wa Simba aliyefunga mabao 19.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic