September 30, 2016

Huyu ni Mtanzania, Shekhan Rashid, mmoja wa viungo bora kabisa ambazo Simba waliwahi kuwapata.

Mmoja wa viungo bora ambao walikuwa wanaijua kazi yao uwanjani na huenda sasa ni vigumu kuwapata wa aina yake.

Kwa sasa Shekhan anacheza soka lakini si la kiushindani kama ilivyokuwa awali na zaidi anaendelea na maisha yake nchini Sweden.

Shekhan anatokea Magomeni Kagera jijini Dar es Salaam, baba wa watoto wawili ambaye anaendesha maisha yake katika jiji la Stockholm.

Shekhan ni mtaratibu, asiyependa makuu na uchezaji wake zaidi ulilenga kusaidia timu. Kwa viungo ambao waliwahi kumuona anacheza, wanaweza kujifunza mengi. Lakini hata maisha yake baada ya soka, yanaonyesha ni mtu anayependa kufanya yaliyo sahihi na asiyependa makuu.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV