September 30, 2016


Mfumo  mpya wa utumiaji wa tiketi za elektroniki kwenye Uwanja wa Taifa, Dar, unatarajiwa kuanza kutumika rasmi kesho Jumamosi katika mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na Simba, lakini tayari kuna malalamiko juu ya tiketi hizo.

Juzi Jumatano ambapo tiketi hizo zilianza kuuzwa katika maeneo mbalimbali, mashabiki wa soka walikuwa wakilalamika utaratibu mbovu wa jinsi ya kuzipata, hali iliyosababisha kutinga kwenye ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), kwa lengo la kujipatia tiketi, lakini wakaambulia patupu.

Kutokana na mvurugano huo, juhudi za kumtafuta Meneja Miradi wa Kampuni ya Selcom inayosimamia mchakato huo, Gallus Runyeta, zilifanyika na yeye akutoa ufafanuzi hivi:

“Sasa hivi zoezi linakwenda vizuri bila ya tatizo lolote, ni kweli siku ya kwanza kulikuwa na shida kidogo kutokana na jambo lenyewe kuwa geni katika soka letu, lakini tunashukuru tumefanikiwa kuweka mambo sawa.

“Baada ya kutokea kilichotokea siku ya kwanza ambapo zoezi lilianza mchana, hapohapo watu wasiotupenda wameanza kuuponda mfumo huu mpya, hawa ndiyo wale ambao wameathirika ambao sasa hivi mirija ya kujipatia fedha kijanja imezibwa na lazima watakuwa hawatupendi wakitaka mfumo usitishwe.

“Niwahakikishie zoezi linakwenda bila ya tatizo lolote na wakienda kwenye vituo vyote watazipata, siku ya mchezo bado haijafika, waache kuwa na presha, tumejipanga kikamilifu kufanikisha hili jambo.”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic