September 6, 2016Kipa mkongwe nchini Ivo Mapunda ameamua kutoa machungu yake kwa viongozi, wachezaji na mashabiki wa Simba kuhusiana na kushindwa kumuunga mkono kipa wao Peter Manyika .

MANYIKA PETER (KULIA) WAKATI AKIFUNDISHA SOKA NCHINI OMAN

Kipa huyo wa zamani wa Yanga, Simba, Azam FC ametupia maneno yake kuonyesha hisia zake kwenye mtandao wa kijamii akisisitiza na kukemea.


Peter ambaye ni mtoto wa kipa mkongwe wa zamani wa Yanga, Mtibwa Sugar na Taifa Stars, Manyika Peter, alifiwa na babu yake ambaye ni baba wa kipa huyo wa zamani mkongwe.

IVO WAKATI AKIWA SIMBA

Kwa mujibu wa Ivo Mapunda, amesema ameshangazwa kuona hakuna kiongozi, mchezaji au hata shabiki maarufu aliyejitokeza kumuunga mkono Peter ambaye alikuwa amevaa jezi za Simba full siku ya msiba.


Manyika, ameusifia uongozi wa Yanga kuonyesha ushirikiano mkubwa wakati wa msiba wa baba wa kipa Deugratius Munishi huku akimpongeza Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ambaye alijitokeza hadi kanisani siku hiyo kuungana na Dida na ndugu zake, marafiki pamoja na Wanayanga wengine waliojitokeza.

MANYIKA PETER KAZINI SIMBA

Ivo amekwenda mbali zaidi hadi kufikia kukumbushia viongozi wa Simba kushindwa kujitokeza msibani alipofiwa na wazazi wake wote kwa nyakati tofauti wakati akiitumikia timu hiyo.

2 COMMENTS:

  1. Uhuru wa kuongea una matatizo sana

    ReplyDelete
  2. sio baba hata kaz ya kawaida ya ya utumishi sijui kama inamzungumzia babu. naona anawasifia yanga kwenda kwa DIDA aliyefiwa na baba mzazi mbona hajawasifia hao yanga kwenda kwa KASEKE aliye fiwa na babu kama ilivyo kwa manyika tena misiba yao ilitokea siku moja kaseke alienda peke yake kwa babu yake.SHAME ON YOU TOO.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV