September 6, 2016


Pamoja na mambo mengine, Kocha Mkuu wa Azam FC, Zeben Hernandez anaonekana kujikita zaidi katika masuala ya kiufundi ndani ya uwanja.

Zeben raia wa Hispania mara kwa mara, amekuwa akiwanoa wachezaji wake kwa kutumia ubao akionyesha anataka wacheze vipi.

Kikubwa, amekuwa akisisitiza kupunguza na ikiwezekana kuyaondoa kabisa makosa kwa lengo la kufanya vizuri.

Kocha huyo, anaonekana kuwekeza zaidi kwenye ufundi huenda baada ya kuridhishwa na fiziki ya kikosi chake ambayo hufanywa na wasaidizi wake ambao pia ni raia wa Hispania.

Azam FC iko mjini Mbeya ambako kesho itakuwa na kazi ngumu dhidi ya wakali Prisons FC ambao huwa hawatabiriki.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV