Mashabiki takribani 58 waliotuma maoni yao kuhusiana na kikosi cha Yanga kwenye blog hii, wamesisitiza kwamba kikosi chao lazima kijiimarishe katika kiungo.
Mashabiki hao wanaonekana kuingiwa hofu kutokana na kikosi hicho kupoteza mechi dhidi ya Stand na kiungo kikionekana kimepwaya huku wakiwa wanakutana na Simba, inayoonekana kuwa na kiungo bora zaidi.
Simba inaonekana kuwa na wachezaji wengi vijana zaidi na kiungo bora zaidi. Hali iliyoonyesha kuwapa hofu kubwa mashabiki hao.
"Hii ni hatari sana, lazima kocha Pluijm aifanyie kazi. Unajua hawa jamaa (Simba), wako vizuri sana katika kiungo," alisema Abdul Rashid wa Buguruni jijini Dar es Salaam.
Paul Matiku James wa Geita, naye alisema" "Stand walitupa shida kwenye kiungo. Kilikufa kabisa, sasa tunakutana na Simba. Nina hofu sana."
Wengine walielezea kuhusiana na timu yao kutoonekana ina makali mbele kama ilivyozoeleka.
Hata hivyo, Kocha Hans van der Pluijm, tayari alishaueleza kwamba watahakikisha wanafanya mabadiliko kwa walichoona ni tatizo.
Tayari Yanga ipo mjini Pemba ikijiandaa na mechi dhidi ya Simba itakayopigwa Jumamosi ya Oktoba Mosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment