September 28, 2016


Na Saleh Ally
Kocha Zeben Hernandez wa Azam FC, aligeuka kuwa gumzo hasa wiki iliyopita baada ya timu yake kukutana na kipigo cha pili cha ligi baada ya mechi tano.

Mechi dhidi ya Ndanda FC ilikuwa ya sita, wakapoteza kwa mabao 2-1. Lakini kabla ya hapo walikuwa wamekutana na kipigo kingine cha bao 1-0 kutoka kwa Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kabla, Azam FC ilianza Ligi Kuu Bara kwa sare ya bao 1-1 dhidi ya African Lyon, baada ya hapo ikaamka na kuichakaza Majimaji kwa mabao 3-0. Halafu ikaendeleza ushindi kwa kuchukua pointi sita jijini Mbeya ikizichapa Prisons kwa bao 1-0 na Mbeya City kwa 2-1.


Gumzo limekwenda kwa kocha huyo kijana, wengi wamekuwa wakimlinganisha na kocha mkongwe aliyetupiwa virago Azam FC, Stewart Hall raia wa Uingereza.

Kwamba Hall alikuwa vizuri zaidi kuliko Zeben wengine wakisisitiza, soka la Hispania haliwezi kuwa na mafanikio Tanzania. Hivyo huenda kocha huyo hafai.

Kila mmoja anaweza kuwa na maoni yake na yakawa na mashiko. Lakini kuna kila sababu ya kuangalia kwamba mazingira aliyonayo kocha huyo na jopo lake yapoje.

Kusema kusajili makocha, mfano wa viungo, kocha msaidizi na kadhalika ni kupoteza fedha, haitakuwa sahihi.


Lakini Azam FC, wanataka kwenda kwa weledi na lazima wakubali kuna mambo muhimu ya kufanya.

Mhispania huyo na wenzake, ameichukua Azam FC ikiwa inakosa mambo mengi sana. Achana na wachezaji walio majeruhi kama Serge Wawa, au Shomari Kapombe ambaye alirejea kabla ya kuumia tena.

Lakini haina wachezaji kadhaa waliokuwa mbele katika kikosi cha Azam FC na mchango wao unakubalika. Mfano Kipre Tchetche ambaye alikuwa akisaidina na John Bocco kuisaidia Azam FC kupata ushindi.




Kinda Mtanzania, Farid Mussa alikuwa katika kiwango bora kabisa. Lakini sasa hana msaada na Azam FC kwa kuwa ameishasaini kujiunga na Tenerife ya Hispania. Anaendelea kubaki kimpya na Azam FC inaendelea kusota.

Waliosajiliwa kuchukua nafasi za Farid na Kipre, nani kati yetu anaweza kusema wanacheza katika kiwango kizuri na bora kinachoweza kufananishwa na wachezaji hao ambao wameondoka.

Kama wanacheza vizuri, nani anaweza kusema tayari wamezoea na wanajua nini cha kufanya kama ilivyokuwa kwa Kipre na Farid. Mbaya zaidi kocha na jopo lake ni wapya.

 Kweli Azam FC wanaweza kuwaona hawafanyi vizuri na kuwafukuza. Lakini pia kuna suala la kutafakari mambo kadhaa kuliko ushabiki utangulie au kulaumus ana ili kuonyesha kujua.


Ndani ya kikosi cha Azam FC, nani anaweza kuwa na uhakika kwamba kila mchezaji mpya alikuwa ni chaguo la Zeben au msaidizi wake. Je, kama wamelektwa na wengine wamefaidika ambao wamo ndani ya klabu hiyo?

 Kama haitoshi, hata hao wachezaji wapya waliosajiliwa. Nao watakuwa wanahitaji angalau muda kidogo ili waanze kuonyesha cheche zao kama kweli watakuwa nazo.

 Hivyo uongozi wa Azam FC unapaswa kuwa makini na kama utaamua mambo kwa papara kwa sababu ya kuonyesha kitu fulani, mfano yenyewe haitaki mchezo na ikiamua inatimua mtu mara moja, basi itakosea.

Ninaamini Azam FC itakuwa na kikosi bora kinachoweza kubadilika. Kuchukua pointi zote sita pale Mbeya di kitu kidogo, wenyewe wamefanya hilo.
  
Maana yake wana kikosi bora ambacho kinahitaji uvumilivu angalau kwa kuwa makocha wenyewe wameonyesha juhudi kubwa za kiutendaji, kama watapewa sapoti wanaweza kufanya kitu lakini uamuzi ukiwa wa hisia, mihemko na kufuat tu kwa lengo akina fulani waone. Si mbali Azam FC utakwama.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic