September 22, 2016

ONGALA

Majimaji ya Songea wako jijini Dar es Salaam, tayari kuivaa Simba Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa.

Pamoja na kuonekana kusua katika mechi zote za mwanzo, Majimaji wanaonekana wamepania kuifunga Simba.

Wamepolekewa vizuri na wadau mbalimbali ambao wangependa Simba ishindwe na kupewa huduma bora kabisa.

Majimaji wamefanya mazoezi kwenye Uwanja wa Gymkhana, hali inayoonyesha kuwa wana maandalizi makini hasa.

Kama hiyo haitoshi, wamekamilisha mipango yao ya kumrejesha kocha wao wa zamani, Kali Ongala.

Ongala ambaye ni mshambuliaji wa zamani wa Abajalo ya Sinza na Yanga, aliondoka baada ya kuiwezesha kubaki Ligi Kuu Bara msimu huu.


Lakini taarifa kutoka ndani ya Majimaji, zinaeleza amerejea na ataanza kuonekana kwenye benchi la timu hiyo Jumamosi.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV