September 22, 2016


Kikosi cha Kilimanjaro Queens kimewasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) na kupokelewa na mashabiki na wadau mbalimbali wa soka nchini.

Mashabiki hao walijitokeza kwa ajili ya Kilimanjaro Queens ambaye wamekuwa ni mabingwa wa Kombe la Chalenji la Cecafa baada ya kuwatwanga Kenya kwa mabao 2-1 kwenye fainali mjini Jinja, Uganda.


Kina dada hao wa Tanzania Bara wameweka rekodi ya kuwa mabingwa wa kwanza wa michuano ya Chalenji kwa wanawake.
0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV