September 28, 2016Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji ameonekana “hataki mchezo” baada ya kukabidhi hati kabla ya kuanza ujenzi wa mazoezi wa kikosi cha Yanga.

Uwanja huo wenye ekari 715 uko katika eneo la Gezaulole jijini Dar es Salaam na Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alikuwepo katika hafla hiyo fupi.

Wakati Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Yanga, Mama Karume pia alikuwa kati ya waliohudhuria shughuli hiyo akiambatana na mjumbe wa bodi hiyo, jabir Katundu.


Ujenzi utakapokamilika, Yanga itakuwa na uwanja wake wa mazoezi ambao unatarajia kuwekewa nyasi bandia.

Baada ya kukabidhiwa Mama Karume alisema: “Nilizungumza na Manji, nikamuambia  kuendelea kufikiria Kaunda ni kujidanganya. Wenzetu Simba wanakwenda Bunju, sisi twende Kigamboni. Unajua maana ya Geza Ulole ni Jaribu Uone, tukiwa na uwanja huku, kila atakayejaribu kuja tutamfunga,”alisema na kupata makofi ya pongezi.


Mama Karume alimpongeza Manji kutokana na hatua yake hiyo na kusisitiza ni jambo bora la kuungwa mkono.

Kwa upande wa Waziri Nchemba alimshukuru Mama Karume, pia akampongeza kutokana na ushirikiano wake na namna anavyopambana kwa ajili ya klabu.

“Tukushuru sana, tunajivunia namna unavyolibeba suala hili kwa uzito tangu ujana wako, tena bila kuchoka,” alisema.

Pia Mwigulu alipongeza na kusema: “Hii zawadi ya Manji ni chachu ya mwanzo kabisa kabla ya Jumamosi wakati tunakwenda kupambana na Simba. Iwe chachu cha ushindi.”


“Lakini huu ni wakati wa kuwa na Yanga bora zaidi, kwa kuwa tutakuwa na uwanja na kupata uwezo wa kupambana na akina Al Ahly, TP Mazembe na wengine kwa ushindani sahihi hasa.”a

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV