September 28, 2016Timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 17, Serengeti Boys wametua mjini Brazzaville kwa ajili ya mapambano.

Zimebaki dakika 90 Serengeti Boys wafuzu kucheza Kombe la Mataifa Afrika kwa vijana.

Wataingia uwanjani wikiendi hii wakiwa na faida ya ushindi wa mabao 3-2 jijini Dar es Salaam.

Lakini Congo ambao wana vijeba, wanaonekana kuwa wazuri ambao wanawalazimu Serengeti Boys kukaa imara kwelikweli.

Serengeti Boys wametua  Congo wakitokea Kigali nchini Rwanda ambako waliweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mechi hiyo ya marudiano.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV