September 2, 2016


USTAADHI...
Mashirikisho ya ngumi za kulipwa Tanzania, TPBC Limited, PST na TPBO kwa pamoja yamemuomba Katibu Mkuu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Mohammed Kiganja kuwapa barua rasmi za matamko yake ndani ya siku tatu kuhusiana na vyama hivyo kwa madai anawachafua kwa wadau wao wa kimataifa. 

Vyama hivyo vimeeleza kusikitishwa kwao na madai hayo ya Kiganja aliyenukuliwa na vyombo mbalimbali vya habari, wakidai taarifa hizo zinawafikia washirika wao wa kimataifa wenye nia ya kusaidia mchezo wa ndondi nchini.

Rais wa TBPO, Yassin Abdallah ‘Ustaadh’ alisema wameamua kutoa siku hizo ikiwa ni ushauri waliopewa na mwanasheria wao ambaye wamemteua kusimamia kazi zao kwa pamoja.

“Tumekuwa tukimpigia simu ili kupata ufafanuzi kuhusu matamko yake lakini tunashangaa simu zetu hazipokei na hatujui kuna kosa gani tumelitenda kwake, amekuwa akidai kuwa haturuhusiwi kuratibu mchezo wa ndondi, na tunapaswa kuchukua vibali kutoka TPBC kitu ambacho siyo sahihi. 

“Makampuni yetu yamesajiliwa kihalali kabisa kwa kufanya kazi ambazo yeye anasema sisi haturuhusiwi na tunaomba tupewe hizo barua ndani ya siku tatu,” alisema Ustaadh.

Uamuzi huo wa BMT unaonekana kuwashangaza watu wengi wanaojua masuala ya mchezo wa ngumi na wengi wameanza kuamini kuwa viongozi wapya wa BMT si wanamichezo.

SOURCE: CHAMPIONI


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV