September 29, 2016


Kikosi cha taifa cha vijana, Serengeti Boys kimeendelea na mazoezi yake kama kawaida jijini Brazzaville nchini Congo.

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas Mapunda amezungumza na SALEHJEMBE usiku huu na kusema vijana wanaendelea vizuri kabisa kabisa na ari iko juu.

“Hakika hadi sasa hakuna shida yoyote, vijana wako katika hali nzuri na mambo yanakwenda kama yalivyopangwa.

“Kuhusiana na ari, iko juu na vijana wako tayari kwa ajili ya kazi hiyo Jumapili,” alisema Mapunda.

Boys wanashuka dimbani Jumapili saa 10 ya huko, yaano saa 12 jioni hapa nyumbani, kuwavaa Congo baada ya Boys kuwa wameshinda kwa mabao 3-2 nyumbani Dar es Salaam.


Mechi hiyo ni kuwania kucheza Kombe la Mataifa Afrika, michuano itakayofanyika nchini Madagascar.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV