September 22, 2016



Baada ya kufanikiwa kupata timu nchini Oman na kuachana na Azam FC, taarifa zinaeleza, mshambuliaji Kipre Tchetche ametoweka nchini humo.

Taarifa zinaeleza kuwa, Kipre ameondoka nchini Oman wakati ligi ikiendelea na kuiacha timu ya Al Nahdha kwenye mataa.

 Mmoja wa marafiki wa karibu aliye nchini Oman, amesema viongozi wa klabu hiyo walikuwa wakilalamika kuhusiana na raia huyo wa Ivory Coast.

“Ameondoka na wanalalamika sana, sijui ni kwa nini. Wanalalamika kwa kuwa hawajui sababu na taarifa zinasema yuko kwao Ivory Coast,” alisema.

Juhudi za kumpata nchini Ivory Coast kupitia simu ya mkononi, zilikuwa mtihani ingawa uthibitisho ulipatikana kwamba ana mpango wa kuondoka zake kwenda kucheza Ulaya.

“Kweli yupo hapa Abidjan. Kipre ana mpango wa kwenda Ulaya, ingawa hatujajua ni nchi gani,” alisema rafiki yake wa karibu ambaye alianika awali uamuzi wake wa kucheza Oman.

“Amepata timu na kule Oman hakufurahia hali ilivyo na mazingira. Sasa anashughulikia visa, halafu atakwenda Ulaya. Nitawaambia,” alisema rafiki huyo.

Kipre aliondoka nchini wakati wa mapumziko lakini hakurejea Azam FC, taarifa zilizoelezwa kutoelewa na mmoja wa viongozi wa klabu hiyo.


Baada ya kuwa na taarifa huenda angetua Yanga, baadaye alisaini Al Nahdha ya Oman ambayo huvaa jezi ya kijani na nyeupe. Lakini mwisho, sasa amerejea Ivory Coast.

Juhudi za kuendelea kumtafuta Kipre ili atoe ufafanuzi kuhusiana na hili kwamba anakwenda Ulaya, au anataka kurejea Tanzania na itakuwa timu gani, zinaendelea.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic