September 25, 2016


 Wabunge mashabiki wa Yanga, wamewachakaza wenzao mashabiki wa Simba kwa mabao 5-2 katika mechi ya kuwachangia wahanga wa tetemeko la Kagera.

Katika mechi hiyo iliyopigwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam na Mwigulu Nchemba akawa nyota akifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao. Mohammed Mchengelwa naye alifunga mawili.


Hadi mapumziko, Yanga walikwenda vyumbani tayari wakiwa wanaongoza kwa mabao 5-1, Simba walifunga bao moja katika kipindi cha pili.

Ridhiwani Kikwete naye alikuwa kivutio kutokana na kucheza vizuri katika sehemu ya kiungo na kumpa wakati mgumu Hamisi KIgwangala.


Fedha Sh milioni 187 zimekusanywa katika mechi hiyo ambayo ilitanguliwa na mechi kati ya Bongo Movie dhidi ya Bongo Fleva, pia mechi ya netiboli.

Hadi mwisho, ilikuwa ni bao 1-1 lakini ikalazimika kupigwa mikwaju ya penalti na Bongo Fleva wakashinda kwa penalti 5-4.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mechi hiyo iliyokuwa kivutio. 
SIMBA


YANGA

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV