MPIRA UMEKWISHAAA
-Stand wanachofanya sasa ni mambo mawili, ni kupoteza muda na kubutua mpira
-Tambwe anapiga shuti kali hapa, lakini unakwenda mikononi mwa kipa wa Stand
DAKIKA 5 ZA NYONGEZA
DK 90, Twite anarusha mpira, lakini beki ya Stand wanaokoa na kuwa kona. Inapigwa lakini, goal kick
Dk 87, beki Mlilo wa Stand akiwa chini pale na mpira umesimama tena
SUB Dk 86, Yanga wanamtoa Haji Mwinyi na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima
SUB Dk 85, Stand wanamtoa Kingwande na nafasi yake inachukuliwa na Abaslim Chidiebele
Dk 82, Kingwande anapoteza nafasi nzuri kabisa akiwa uso kwa uso na kipa Barthez, Dante anaokoa vizuri kabisa
Dk 79, Job anafanya kazi ya ziada kuokoa mpira wa Juba Abdul, inakuwa kona. Inachongwa lakini Stand wanaokoa hapa
SUB Dk 77, Ngoma anakwenda nje upande wa Yanga na nafasi yake inachukuliwa na Obey Chirwa
Dk 76 sasa, bado mpira haujatulia, Yanga wanajaribu kushambulia kwa kasi lakini Stand wao wanaonekana kubutua zaidi
KADI Dk 74 Ngoma analambwa kadi ya njano kwa kumtwanga teke Adam Kingwamnde
KADI Dk 72, Frank Khamis wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kubutua mpira baada ya kipenga
SUB Dk 70 Kipa Mhonge wa Stand analambwa kadi ya njano kwa kupoteza muda
Dk 67, Msuva anapiga shuti kali la mpira wa adhabu lakini linapaaa juuu
Dk 65 Krosi ya Bossou, Tambwe anapiga kichwa safi lakini Muhonge, kipa wa Stand kutoka Uganda, anadaka vizuri kabisa huku akiweka mbwebwe
Dk 64 sasa, Yanga wanafanya mashambulizi mfululizo kuhakikisha wanasawazisha
SUB Dk 62, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Juma Mahadhi, mashabiki wa Stand wanaendelea kuimba kwa shangwe
GOOOOO Dk 60, Pastory Athanas anaifungia Stand bao safi kwa shuti kali baada ya beki Haji Mwinyi kutaka kuupata rangi mpira
56, mechi inaendelea baada ya Job kutolewa na wachezaji wa Yanga na Stand wanagongana tena, wako chini pale ni Tambwe na Adeyum
Dk 51, Job anagongana na kipa wake, Muhonge pamoja na ngoma, mpira unasimama, anatibiwa kwa takribani dakika mbili
Dk 47, Yanga wanaanza kushambuliakwa kasi kubwa, lakini Stand wanaonekana kuwa makini
MAPUMZIKO
-Krosi safi ya Msuva, lakini Kaseke anaonekana alifumba macho, mpira wa kichwa aliopiga unakuwa goal kickDAKIKA TATU ZA NYONGEZA
Dk 45, Msuva anafanyiwa madhambi na Ibrahim Job, yuko chini anatibiwa na mpira umesimama
Dk 43, Stand wanagongeana vizuri lakini Dante anakuwa makini na kuondosha hatari
Dk 40, hakuna timu yenye uhakika wa bao hadi sasa na basi zinaonekana kupigwa katikati ya uwanja zaidi
Dk 37, kipa wa Stand United anaudaka kwa ustadi mkubwa mpira wa faulo wa Thabani Kamusoko, lakini analala chini kuwa ameumia
KADI Dk 36, nahodha wa Stand, Jacob Masawe analambwa kadi ya njano kwa kuzuia mpira usichezwe
Dk 35, Yanga wanapoteza nafasi nzuri baada ya Ngoma kuukosa mpira wa kona iliyochongwa na Msuva
SUB Dk 33 Stand wanafanya mabadiliko ya kwanza kwa kumuingiza Frank Khamis kuchukua nafasi ya Jeremia Khatura
Dk 30, ni nusu saa sasa, Stand wanaonekana kushambulia zaidi lango la Yanga.
Dk 29, Stand United wanaonekana kutulia na kuwasumbua sana Yanga. MAshambulizi yao ni makali zaidi na Yanga wanapaswa kuwa makini la sivyo watajilaumu
DK 28, Kelvin Sabato anamtoka Dante na kuingia vizuri, anapiga shuti kali lakini linaokolewa na kipa Mustapha na kuwa kona. Inachongwa, haina manufaa
Dk 24, Msuva anatoa pasi safi kabisa kwa Ngoma, lakini anaugusa mpira kidogo sana unaangukia mikononi mwa kipa
Dk 23, krosi nzuri ya Pastory Athanas lakini barthez anafanya kaz ya ziada kuokoa, kona. Inachongwa na Yanga wanaokoa
Dk 20, Ngoma anapambana na mabeki wawili wa Stand na kunpa pasi Tambwe lakini anapiga shuti kuuubwaa
Dk 19, Yanga wanagongeana vizuri, mpira unamfikia Kamusoko, anapiga shuti lakini kipa anadaka vizuri
Dk 16, Yanga wanaingia vizuri, Msuva anajaribu kuuwahi mpira, hata hivyo anadhibitiwa
Dk 14, Kimngwande anawatoka mabeki wawili wa Yanga akiwemo Bossou, lakini hata hivyo kasi yake inakuwa ndogo
Dk 12, nafasi nzuri kabisa kwa Stand United lakini Adam Kingwande anapoteza akiwa amebaki yeye na Mustapha
DK 8, mpira unakwenda taratibu sana na hakuna timu inayoonyesha kupatia kupata bao.
Dk 5, beki Adeyum Saleh wa Stand anajigonga kwa Msuva na kuanguka, anatibiwa hapa na baadaye anarejea. Kidogo alianguka vibaya
Dk 3, hadi sasa hakuna shambulizi kali upande wowote, Yanga wamepata kona lakini bado haikuwa na madhara yoyote kwa Stand
Dk 1, Yanga ndiyo wanakuwa wa kwanza kufika katika lango la Stand United, lakini inaonekana wachezaji wa Yanga, waliishaotea.
0 COMMENTS:
Post a Comment