September 26, 2016


Baada ya kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa wakata tiketi wa Stendi ya Shinyanga, Stand United, Kikosi cha Yanga kinatarajia kuendelea kuweka kambi mkoani Shinyanga au kinaweza kwenda mkoa jirani, Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mechi yake dhidi ya watani wao wa jadi, Simba itakayochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Yanga, Baraka Deusdedit, alisema kikosi chao kinatarajia kuendelea kuweka kambi mkoani humo kabla ya kurejea kwa ajili ya kuikabili Simba Oktoba Mosi.

“Kikosi chetu kitaendelea kuweka kambi mkoani Shinyanga au kitakwenda Mwanza kwa ajili ya kujiandaa na mechi yetu dhidi ya Simba ambapo kitarejea siku chache kabla ya mchezo.


“Mchezo wa Simba ni wa kawaida kwetu na tunajiandaa kama ilivyo kwa mechi nyingine kwani tumeshakutana na timu kubwa ikiwemo TP Mazembe, hivyo tunaupa uzito sawa mchezo huo na ile mingine,” alisema Baraka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV