September 26, 2016



Kiungo na nahodha wa Simba, Jonas Mkude, amesema ushindi mnono wa mabao 4-0 walioupata juzi Jumamosi mbele ya vibonde, Majimaji ni salamu tosha kwa timu yoyote ambayo haijakutana na moto wao, ikiwemo Yanga ambayo watakutana nayo Jumamosi hii.

Simba imeanza ligi kwa moto wa gesi, ikiwa kileleni na jumla ya pointi 16 katika mechi sita ilizocheza, ikifuatwa na Yanga ambayo kabla ya mchezo wa jana ilikuwa na pointi 10.

Mkude amesema mwendokasi wanaokwenda nao ndiyo kama kauli mbiu msimu huu kwani wamedhamiria kufuta ukame wa mataji Msimbazi.

Ikumbukwe Yanga iliiadhibu Simba mara mbili msimu uliopita kwa kuichapa mabao 2-0 kila mchezo, lakini Mkude anasema ni kama waliwaotea kwa kutumia makosa lakini safari hii hawataki kufanya uzembe.

“Soka ni mchezo wa makosa, unapofanya kosa ni lazima ujutie. Sisi tulifanya makosa wakayatumia vema, ndiyo maana nasema ni lazima tuwe makini kutorudia makosa kama yale ili kutimiza azma yetu (ubingwa),” alisema nahodha huyo.

Mwendokasi wa Simba ya sasa umechagizwa zaidi na viberenge, Shiza Kichuya, Mohamed Hussein Zimbwe ‘Tshabalala’, Jamal Mnyate, Yassin Mzamiru na Ibrahim Ajibu.

“Kweli wana kasi kubwa na ninafikiri itasaidia kwa kiasi kikubwa Simba kufanya vizuri zaidi kwenye mechi zijazo,” aliongeza.


Aidha, kichapo cha juzi kwa Majimaji, ni mwendelezo wa kuboronga chini ya kaimu kocha mkuu, Peter Mhina ambapo imepoteza mechi zote sita, hata hivyo jana Jumapili uongozi wa timu hiyo ulikuwa umalizane na aliyewahi kuwa kocha wao, Kally Ongala ili kuinusuru.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic