September 28, 2016Kocha wa zamani wa Simba, Muingereza, Dylan Kerr, kwa sasa anakula maisha nyumbani kwao baada ya kupewa vyeo viwili vya juu tangu alipotimuliwa kwenye benchi la ufundi la Simba, msimu uliopita.

Kerr ambaye alipewa mkataba wa miaka miwili wa kuinoa Simba mwanzoni mwa msimu uliopita, mkataba wake ulikuja kuvunjwa akiwa ameutumikia miezi sita tu baada ya matokeo mabaya aliyokuwa akiyapata kwenye Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Mapinduzi ambapo Simba iliondolewa hatua ya nusu fainali na Mtibwa Sugar.

Baada ya kuchana na Simba Januari, mwaka huu, Kerr hakuwa na kazi maalum mpaka hivi karibuni alipopewa majukumu  ya kuinoa timu ya Chuo cha Leeds, pamoja na kuwa skauti mkuu wa Klabu ya Doncaster Rovers inayoshiriki Ligi Daraja la Pili England, ambayo inanolewa na mtoto wa kocha wa zamani wa Manchester United, Sir. Alex Ferguson, Darren Ferguson.


“Rafiki yangu sasa hivi nipo hapa nyumbani nikifanya kazi zangu za ukocha ambapo ninaifundisha timu ya Chuo cha Leeds, lakini pia nimechaguliwa kuwa skauti mkuu wa timu yangu ya mtaani ya Doncaster Rovers, kazi hizi zote nimezianza mwezi uliopita,” alisema Kerr ambaye kila siku amekuwa na ndoto ya kurudi Tanzania kufundisha soka.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV