September 28, 2016



Wakati Yanga ikiendelea kujiandaa na mchezo dhidi ya watani wao wa jadi, Simba SC, pia imepokea habari nzuri za kurejea kikosini kwa winga wao hatari, Geofrey Mwashiuya kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi hicho.

Mwashiuya ambaye kwa muda mrefu alikuwa Mbeya akijiuguza majeraha yake ya goti, amejiunga na timu hiyo juzi huko kambini visiwani Pemba, tayari kwa ajili ya kuanza mazoezi mepesi ya kujiweka fiti kabla ya kujumuika na mazoezi ya kikosi.

Mwashiuya ambaye amekuwa akisifika kwa spidi, vyenga na kupiga mashuti, alikuwa nje ya timu hiyo kwa takriban miezi miwili sasa tangu alipoumia lakini sasa kurejea kwake kumemfurahisha kocha wa timu hiyo, Mdachi, Hans van Der Pluijm na kueleza kuhusiana na hilo.


“Ni vizuri kama kijana amerejea na zaidi anaendelea vizuri, tupo naye Pemba na tayari kuna programu ameandaliwa kwa ajili ya kuanza nayo kwanza huku daktari akimuangalia mwenendo wake, kisha baada ya hapo atajumuika na kikosi kizima,” alisema Pluijm.

SOURCE: CHAMPIONI

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic