October 19, 2016Kiungo wa zamani wa timu ya soka ya Simba na Mbeya City,Haruna Moshi ‘Boban’,amewapongeza waandaaji wa tamasha la soka la Kandanda day,lililofanyika Jumamosi katika viwanja vya Jakaya M Park Youth.

Boban,ambaye alikuwa anaiwakilisha timu yake ya Dar City Fc,katika tamasha hilo,alisema amejisikia faraja kuwa mmoja wa watu walioshiriki moja kwa moja katika kuchangia madawati kupitia tamasha hilo.

“Kwakweli nawapongeza sana waandaaji wa tamasha la Kandanda day,ingawa timu yangu ya Dar City haijafanikiwa kushinda mchezo wetu wa fainali,lakini kwetu haikuwa tatizo.

"Kwa kuwa nia ya ushiriki wetu ni kwa ajili ya progarmu maalumu ya kuchangia madawati kwa jamii,kwahiyo kwetu ilikuwa ni jambo muhimu zaidi kuwa sehemu ya mchango kwa jamii kuliko kupata ushindi,” alisema Boban.

Timu hiyo ya Dar City,ambayo ilikuwa ikiundwa na wachezaji mbalimbali wa zamani,katika mchezo wa fainali ambao ulikuwa ni mzuri na wa uliojaa ufundi mwingi,waliangukia pua baada ya kufungwa  na Coca Cola,kwa jumla ya mabao 3 kwa mtungi.

Tamasha la mwaka huu lilimepewa nguvu kubwa na kampuni ya wauzaji matairi ya BinSlum pamoja na Smart,Coca Cola,Galacha,Michuzi Blog,Akiba Commercial Bank (ACB) pamoja kituo cha House of Blue Hope.  

Imetolewa na Mratibu wa tamasha

Mohamed Mkangara

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV