Obey Chirwa amesema yeye ni mfungaji, anataka kuendelea kufunga mabao kwa ajili ya kikosi chake cha Yanga.
Chirwa raia wa Zambia ana mabao matano, anasema anataka zaidi ili kujiongezea morali.
Lakini kama itashindikana kabisa, anachotaka ni kuisaidia timu yake kupata ushindi.
“Nikifunga, timu inapata ushindi. Nisipofunga basi ntajitahidi kuisaidia timu ili ipate ushindi pia.
“Kikubwa kwa pamoja tunataka timu ishinde bila kujali anafunga nani,” alisema Chirwa ambaye ni mtaratibu.
Chirwa amejiunga na Yanga akitokea FC Platnums ya Zimbabwe na alianza kwa ugumu kwa kuwa hakuwa amefunga.
Katibu wa Baraza la Wazee wa Yanga, Ibrahim Akilimali aliwahi kusema hana lolote. Lakini mwisho alipoona ameanza kupachika mabao akasema; “Chirwa ni jembe wewe, nilikuwa namtia upepo tu.”
0 COMMENTS:
Post a Comment