October 31, 2016


Kifo cha bondia maarufu nchini, Thomas Mashali kimetawaliwa na utata mkubwa, kila mmoja akisema lake.

Mashali ameokotwa akiwa amefariki dunia baada ya kuwawa na watu wasiojulikana, lakini hakuna mwenye uhakika ilikuwaje.

Pamoja na hivyo, kumekuwa na taarifa kwamba alikuwa na wenzake, walikwenda kuvamia sehemu kwa ajili ya kuiba kwenye duka la Tigo Pesa.

Taarifa nyingine zinasema Mashali alikwenda kumdai mtu, wakapishana kauli na yule mtu akamuitia watu kuwa ni mwizi na taarifa nyingine zinaeleza kwamba Mashali aliuwawa na watu ambao alizozana nao wakati wakiburudika na kinywaji baa.

Katibu Mkuu wa moja ya mashirikisho ya ngumi za kulipwa nchini la PST, Anthony Rutta amekiri wao kupokea taarifa hizo.

"Ni kweli kuna taarifa zinachanganya sana kama hiyo sijui walikwenda kuiba kwenye Tigo Pesa, wengine wanasema aliitiwa mwizi na mtu anayemdai pia kuna ishu inasema kwamba aligombana na vijana wa Kichaga, wakamshambulia.

"Sasa haijajulikana, tumeamua tuliachie jeshi la polisi lifanye kazi yake. Kama kuna tatizo kwa marehemu au wengine, tutajua," alisema Rutta.

Taarifa za kifo cha Mashali zinaonekana kuwashitua watu wengi ambao walikuwa wanaujua ubora wake na inaelezwa jana alikuwa katika kikao cha mabondia na alieleza machungu yake kuhusiana na mambo mengi ambayo hayakumfurahisha.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV