October 2, 2016


Kikosi cha timu ya taifa ya soka la ufukweni cha Oman, kimeshika nafasi ya pili katika michuano ya bara la Asia.

Oman inayofundishwa na kocha wa zamani wa Simba, Talib Hilal ilipoteza mechi yake ya fainali baada ya kupokea kipigo cha mabao 4-3 kutoka kwa Japan. Kipa wa zamani wa Pamba, Yusuf Abeid ndiye kocha wa makipa wa kikosi hicho.

Katika michuano hiyo iliyomalizika nchini Vietnam, Oman ilianza vibaya lakini ikafanikiwa kutinga fainali.


Katika mechi ya ufunguzi, Oman ilikutana na kipigo cha mabao 3-2 ikiwa ni kwa mikwaju ya penalti kutoka kwa Lebanon lakini haikuwakatisha tamaa.

Baada ya hapo walirejea katika mechi ya pili na kuwagonga Qatar mabao 4-2, halafu robo fainali wakawanyoosha Thailand mabao 4-1 na kutinga nusu fainali.


Katika mechi ya nusu fainali, Oman waliwavaa Afgahinstan ambao walionekana hawatabiriki, lakini wakawachakaza kwa mabao 8-2 na kutinga fainali waliyokutana na Japan ambayo walipoteza kwa tofauti ya bao moja.


Hilal amekuwa na mafanikio makubwa katika kazi ya ukocha katika upande wa ufukweni kwa Oman imekuwa ikishiriki michuano ya Kombe la Dunia na kufanya vizuri lakini chini yake inaonekana pia ni tishio barani Asia na duniani kote.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic