October 2, 2016

WAZIRI NAPE AKIZUNGUMZA NA WAANDISHI WA HABARI AKIWA KWENYE UWANJA WA TAIFA JIJINI DAR ES SALAAM.

Serikali imezuia fedha za mapato ya mechi kati ya Simba dhidi ya Yanga hadi hapo gharama za uharibifu wa viti katika mechi yao dhidi ya Yanga, itakapojulikana.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye amesema kwamba Simba inatakiwa kulipa gharama ya viti 1,781 vilivyoharibiwa na mashabiki wake.

Nape amesisitiza, fedha za mapato ya Simba zitaendelea kushikiliwa hadi hapo suala la gharama ya uharibifu itakapojulikana.

"Gharama ikijulikana, watakatwa mara moja. Na kama haitoshi, basi watalipishwa zaidi," alisema.

Tayari kupitia Nape, serikali imetangaza kuzifungia Yanga na Simba kuutumia uwanja huo hadi hapo baadaye.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja huo, jana ikiwa ni baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao.


Tambwe raia wa Burundi, alifunga bao hilo baada ya kuunawa mpira, jambo ambalo lilisababisha tafrani hasa baada ya yeye kwenda kushangilia upande wa mashabiki wa Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic