MPIRA UMEKWISHAAA
-Muzamiru ameumia, anatolewa nje kwa ajili ya matibabu, Simba wanacheza pungufu kwa kuwa wamemaliza sub
-Ame anapata pasi nyingine nzuri ya Ajibu, abapiga shuti kuuubwaaa
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, Angbani analazimika kuokoa mpira safi wa kichwa wa Hamisi, inakuwa kona tena. Inapigwa na Angbani anadaka kwa ufundi kabisa
Dk 88, Ame Ali anapata nafasi nzuri lakini anaichezea kwa kutaka kupiga chenga
Dk 86 sasa, inaonekana kama Simba wameridhika na mabao hayo matatu, wanapiga pasi hapa na pale wakiwa hawana hofu na Mwadui bao kama hawana presha sana, kama vile wamethibitisha kufungwa
Dk 81, Ame Ali anapiga kichwa lakini hakulengaDk 77, Nonga tena anajaribu lakini shuti lake linatoka pembeni mwa lango
Dk 72 Mwadui wanafanya shambulizi jingine hapa lakini shuti la Nonga linatoka nje
SUB Dk 66 Simba wanamtoa Kichuya, nafasi yake inachukulwia na Said Ndemla
SUB Dk 63, Kado anakwenda nje baada ya kushindwa kuendelea
Dk 62, Kado anaonekana ameshindwa kuendelea. Daktari anaingia tena na kuanza kumtibu, inawezekana MWadui watafanya mabadiliko
SUB Dk 57 hadi 60, kipa Kado anatibiwa hapa uwanjani baada ya kubanwa msuri. Mpira unaendelea sasa
Dk 55, Muzamiru anaingia vizuri na kupiga shuti kali hapa, kona. Inachongwa lakini haina madhara
Dk 52, kipa Shabani Kado anatoka kasi na kuokoa vizuri kabisa
GOOOOOOOOO Dk 50, Mo Ibrahim anaifungia Simba bao tena, anaunganisha vizuri pasi safi kabisa ya Ame Ali
Dk 49, Nonga anadanganya, anaingia vizuri anapiga shuti, nje
Dk 48, MWadui wanapata kona yao ya kwanza kipindi cha pili, inachongwa na Ismail, haina matunda
SUB Dk 46, Ibrahim Ajibu anaingia uwanjani kuchukua nafasi ya Mwinyi Kazimoto, mpira umeanza
MAPUMZIKO
GOOOOOOOOO Dk 45, Kichuya anaifungia Simba bao la pili leo, la nane kwake akiunganisha pasi safi ya Mohamed Ibrahim
Dk 44, Rajab Ismail anaingia vizuri hapa, anapiga shuti hatari. Lakini linatoka kidogo tu nje ya lango la Simba
SUB Dk 42, Simba wanafanya mabadiliko, wanamtoa Mavugo na nafasi yake inachukuliwa na Ame Ali
Dk 40 sasa, bado mpira haujachangamka sana, Simba wana mashambulizi kadhaa lakini si makini katika umaliziaji na MWadui FC wanaonekana kutokuwa na mipango bora wanapofika kwenye lango la Simba
Dk 35, hatari kwenye lango la Mwadui, Kazimoto anamtoka kipa na kumpa Muzamiru pasi peke yake na nyavu, anaukosa mpira unaokolewa
DK 33, Mwadui wanaingia vizuri, shuti la Madenge lakini linamgonga Angban usoni na Mwanjale anaokoaGOOOOOO Dk 32, Mo Ibrahim anamchambua beki wa MWadui na kufunga bao safi kabisa kwa Simba
Dk 31, pasi nzuri ya Kazimoto, Mo Ibrahim anashindwa kuitumia na kupiga shuti nyanya hapa
Dk 29, MWadui wanapata kona ya kwanza hapa, inachongwa vizuri na Rashid Ismail anajitwika lakini inakuwa ni goal kick
Dk 25, Mavugo anatoa krosi safi kabisa kwa Kichuya, lakini anaruka na kupiga kichwa juuuu
Dk 22 sasa, mpira hauvutii sana, hakuna timu inayoonyesha imepania kupata mabao ya haraka. Zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja na hakuna mashambulizi makali
Dk 14, Rashid Ismail anapiga shuti karibu kabisa na langu la Simba, unapita juu
Dk 9 Mwadui wanapoteza nafasi nyingine ya wazi hapa baada ya kupiga shuti kuuubwa
Dk 9, MWadui wanagongeana vizuri wanafunga hapa lakini Hamisi alikuwa ameishaotea
Dk 7, Mavugo tena anaichezea nafasi nyingine na kupiga juu akiwa na nafasi nzuri kama angetulia
Dk 6, Mavugo anawachambua mabeki wa Mwadui na kuachia mkwaju mkali, unatoka juu kidogo
Dk 4, bado hakuna kitu chochote ambacho kinaonekana ni mabadiliko kwa kuwa mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja.
Dk 1 Simba wameanza kwa kasi lakini shuti la Mavugo linatoka nje.
1. Vicent Angban
2. Janvier Bukungu
3. Mohamed Zimbwe
4. Method Mwanjale
5. Juuko Murshid
6. Jonas Mkude
7. Mzamiru Yassin
8. Mwinyi Kazimoto
9. Laudit Mavugo
10. Shiza Kichuya
10. Shiza Kichuya
11. Mohamed Ibrahim
Sub
Manyika
Hamadi
Novart
Ndemla
Ndusha
Ajib
Ame
0 COMMENTS:
Post a Comment