October 1, 2016


MPIRA UMEKWISHAAAA
-Kona ya Yanga, Haji Mwinyi anaruka hapa na kupiga kichwa, nusura aipatie Yanga bao inakuwa gaoal kick

DAKIKA 3 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanaendelea kushambulia, lakini Yanga hawajalala nao wanajibu mashambulizi
GOOOOOOOOOOOO Dk 87, Simba wanapata kona safi baada ya krosi ya Bukungu. Inachongwana Kichuya, 

Dk 85 Juma Abdul krosi yake iipatie Yanga bao baada ya Tambwe kupiga kichwa safi kabisa
Dk 84, mpira mzuri kabisa wa Mwanjale, Simba wanaingia vizuri lakini mawasiliano ya Mo Ibrahim na Blagnon yanaonekana kutokuwa mazuri
Dk 83, Yanga wanaingia vizuri hatari kwenye lango la Simba, wapi wanaokpoa hapa
SUB Dk 81, Msuva anaingia kuchukua nafasi ya Juma Mahadhi
SUB Dk 79, Yanga wanamtoa Kaseke na nafasi yake inachukuliwa na Haruna Niyonzima.
KADI Dk 77, Barthez analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha muda
SUB Dk 77, Simba wanamtoa Ajib na nafasi yake inachukuliwa na Mohamed Ibrahim
Dk 76, Kazimoto anageuka na kupiga shuti kali kabisa hapa, lakini ni goal kick
Dk 74, Simba wanapata kona, inachongwa lakini Yanga wanaokoa kwa ulaini kabisa kupitia Dante hapa
Dk 71, Juuko anaachia mkwaju  mkali kwelikweli, mpira unapita juu kidogo kwenye lango la Yanga, goal kick
KADI Dk 71, Twite analambwa kadi ya njano baada ya kumlamba ngwara Kazimoto
KADI Dk 69, Zimbwe Jr analambwa kadi ya njano kwa kucheza faulo
DK 67, Yanga wanapata kona hapa na inakwenda kuchongwa na Haji Mwinyi. Goal Kick, Haji alijaribu shuti lakini limepaa buuu

Dk 64, Tambwe anawachambua mabeki wa Simba na kutoa krosi safi hapa lakini Simba wanaokoa katikati hapa
SUB Dk 62, Simba wanawatoa Lufunga anaingia Juuko Murshid, pia wanamtoa Mavugo na nafasi yake anachukua Blagnon Frederic
Dk 60 sasa, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza taratibu kabisa huku Simba wakionekana kuhaha na hawajatulia kabisa
Dk 58 sasa, timu bado zinashambuliana kwa zamu, Simba wanakuwa na tatizo la kupoteza pasi mara kwa mara
Dk 55 Kazi ipo, Lufunga na Tambwe hapa, Lufunga anampitia Tambwe, yuko chini anatibiwa hapa
Dk 53, Simba wanashambulia, Kichuya anaingia na kupiga shuti kali lakini kuuuubwaaa
Dk 51,, Tambwe yuko chini, inaonekana kama Lufunga alirusha mkono wake ukampata usoni

Dk 50, Zimbwe Jr anafanya kaosa hapa, Kaseke anaingia anapiga kwosri hapa lakini Angban anadaka vizuri
Dk 49, Bukungu anapiga shuti kali ule mpira wa faulo, unagonga mwamba na kurudi, Mavugo anapiga shuti lakini unaokolewa
DK 48, Kichuya anawachambua mabeki wa Yanga, wanamuangusha inakuwa faulo
SUB Dk 47 Yanga inamtoa Yondani na nafasi yake inachukuliwa na Andrew Vicent au Dante
 Dk 46, Simba wanaanza kwa kasi, Mwinyi anaingia na kumuangusha Kichuya hapa-

MAPUMZIKO
-Ajibu anawalamba chenga mabeki wa Yanga na kuachia shuti kali lakini ni goal kick
-KADI Yondani analambwa kadi ya njano baada ya kuchelewesha mpira
Dk 45 Kipa Barthez yuko chini pale akitibiwa baada ya kugongana na Juma Abdul baada ya kugongana
Dk 45, Mavugo anaingia vizuri, anamtola Juma Abdul na kupiga shuti, BArthez anaokoa na kuwa kona. 
Dk 44, Yanga wanashambulia tena shuti hapa la Mahadhi lakini linakuwa dhaifu
Dk 43, Mavugo anajaribu shuti lakini linatoka nje sentimeta chache
Dk 42, Tambwe yuko chini pale baada ya kuangushwa na mwamuzi anaonya pale
Dk 40, Kichuya anaingia vizuri kabisa anaachia shuti kali lakini halikulenga lango
Dk 37, Ngoma anawachambua mabeki wa Simba kama karanga hapa na kuachia shuti kali kabisa, lakini Angbani anadaka vizuri
Dk 30 hadi 35, mpira unachezwa zaidi katikati ya uwanja hata hivyo Simba wanaonekana hawajatulia baada ya kulalamikia lile bao la Tambwe ambaye alishika na kulalamikiwa na wachezaji hao

Dk 29, mpira bado umesimama, mashabiki wa Simba wanang'oa viti, polisi wanapiga mabomu ya machozi
KADI Dk 28 Mwamuzi anamlamba kadi nyekundu nahodha wa Simba Jonas Mkude, haijajulikana kama alifanya nini
Dk 27, walinzi wanalazimika kuingia uwanjani kuwapoeza wachezaji wa Simba wakilalamika kama wanasusia baada ya Tambwe kufunga bao hilo wakisema alishika GOOOOOOOOOOOO Dk 26, Tambwe anaipatia Yanga bao safi baada ya kugeuka na mpira ukiwa mkononi mbele ya Lufunga na kufunga kirahisi kabisa
Dk 24, Mpira wa kurushwa, Ajibu anaunganidha shuti juujuu hapa lakini anashindwa kulenga lango na mashabiki wa Yanga wanazomeee buuuuuu

Dk 23, Kichuya anaangushwa hapa, mwamuzi anasema faulo lakini yeye analalmika huku upande mwingine Bossou naye akiwa analalamika kwamba amepigwa kiwiko
Dk 22, Ajibu anajaribu kuwachambua mabeki wa Yanga, anaanguka lakini mwamuzi anamwambia amka twende kazini baba
 Dk 20, Simba wanagomngeana vizuri zaidi lakini wanakuwa si wazuri katika kumalizia
Dk 16, Yanga wanaonekana kutulia zaidi na kucheza soka safi zaidi huku Simba wakihaha kuwakapa
Dk 14, Krosi nzuri ya Juma Abdul, Kamusoko anapiga kichwa kinatoka sentimeta chache nje juu ya lango la Simba

Dk 11, Mavugo anawekwa chini na Yondani, anatibiwa na kutolewa nje. Mpira unaendelea
Dk 9, mpira wa faulo wa Mavugo, unababatiza ukuta wa mabeki wa Yanga na kuokolewa
Dk 7, Zimbwe anatelekeza lakini anauwahi mpira na kuutoa, inakuwa kona,inachongwa
hatari hapaa, shuti la Tambwe linatoka sentimeta chache kabisa
Dk 6, Kichuya anatoa pasi nzuri kwa Ajib, anageuka na kupiga, mpira unaingia langoni. Lakini mwamuzi Saanya anasema ilikuwa offside tayari
DK 3, Kazimoto anaangushwa wakati akienda kufunga, mwamuzi anasema faulo, anaipiga Ajibu lakini juuuuu
Dk 1, mechi imeanza taratibu na Yanga wanakuwa wa kwanza kufika kwenye lango la Simba.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic