October 5, 2016Simba imepigwa faini ya Sh milioni 5 kutokana na mashabiki wake kung’oa viti vya Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam, Jumamosi.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati timu yao ikicheza na Yanga ikiwa ni baada ya mshambuliaji Mrundi, Amissi Tambwe kufunga, lakini kabla alikuwa ameshika mpira.

Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imefikia uamuzi wa kuipa Simba adhabu hiyo.

Kama hiyo haitoshi, kamati hiyo imeionya Simba kwa kusisitiza ni onyo kali na kama itatokea tena itatoa adhabu kali.

Moja ya adhabu ambazo zimetajwa ni pamoja na Simba kucheza bila ya mashabiki.


Msisitizo wa kamati hiyo, umesema adhabu hiyo imetolewa kutoka kwa mujibu wa kanuni ya 42(3) na 24(7) za Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV