October 5, 2016


Kadi nyekundu aliyolambwa nahodha wa Simba, Jonas Mkude imefutwa.

Kamati ya Bodi ya Ligi ya uendeshaji na Usimamizi wa Ligi iliyokaa jana, imefikia uamuzi wa kwamba inaonekana Mkude hakuwa na tatizo.

Mkude aliingia kwenye mzozo na mwamuzi Martin Saanya baada ya kukubali bao la Amissi Tambwe wa Yanga ambaye kabla ya kufunga, aliushika mpira.

Hiyo ilikuwa katika mechi ya watani, Yanga na Simba ambayo iliisha kwa sare ya bao 1-1.


Uamuzi wa kamati hiyo, unamrejesha Mkude mchezoni wakati Simba ikisafiri kwenda Mbeya kwa ajili ya kuivaa Mbeya City, wiki ijayo.

1 COMMENTS:

  1. Ni Simba pekee ambao kadi nyekundu inaweza kufutwa au mchezaji kuchagua au timu kuchagua ni mechi ipi ya kutumikia adhabu ya kadi za njano.

    ReplyDelete

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV