Mshambuliaji nyota wa zamani wa TP Mazembe, Thomas Ulimwengu ameendelea kujifua mchangani jijini Dar es Salaam ili kuhakikisha yuko fiti.
Ulimwengu ambaye amekataa kusaini mkataba tena na TP Mazembe akiwa ameelekeza malengo yake barani Ulaya, amekuwa akiendelea na mazoezi kujiweka fiti.
Kabla alianza mazoezi ya gym na baadaye alizungumzia taarifa kwamba angefanya mazoezi na Azam FC na kusema asingeweza kufanya mazoezi na timu iliyo kwenye ligi na badala yake anaendelea na programu zake.
Gym ndiyo alianza nayo lakini kukimbia na kufanya mazoezi mengine mchangani imefuatia.
Tayari kuna taarifa mshambuliaji huyo anatakiwa na timu kadhaa barani Ulaya zikiwamo za nchini Ubelgiji ambako Mtanzania mwingine, Mbwana Samatta anakipiga.
Hata hivyo, bado haijajulikana timu ipi itamalizana naye vizuri na wakala wake alitarajia kutua nchini kwa ajili ya kumaliza suala hilo.
0 COMMENTS:
Post a Comment