DULLA MBABE AKIMUANGALIA ZHENG (KUSHOTO), HII ILIKUWA WAKATI WA KUPIMA UZITO, JANA. |
Bondia wa ngumi za kulipwa nchini, Abdallah Pazi ‘Dulla Mbabe’ ameonyesha hataki mchezo baada ya kumchakaza Mchina, Chengbo Zheng katika raundi ya kwanza tu.
Pambano hilo la raundi 10 limefanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam na lilikuwa linasubiriwa kwa hamu kwa kuwa kila bondia alijitapa awali.
Wakati watu walikosa burudani ya pambano la utangulizi la Cosmas Cheka dhidi ya Jason Bedemen raia wa Afrika Kusini ambaye aligoma akidai amebadilishiwa bondia na pambano lake kuondolewa ubingwa, hivyo nguvu zote zikaelekezwa kwenye pambano la Dulla Mbabe na Mchina huyo.
Wakati wengi waliamini pambano litakuwa na ushindani mkali, Dulla alishambulia kwa kasi na kumuangusha Zheng ambaye alijikongoja na kuendelea.
Lakini ikionekana kama atatulia, Dulla alimsogeza kona na kupeleka ngumi nne mfululizo ambazo zilimbaliza na kumaliza pambano kwani baada ya Zheng kwenda chini, hakuweza kuinuka tena na ikawa kwaheri.
0 COMMENTS:
Post a Comment