October 2, 2016Viti vilivyovunjwa na kung’olewa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam ni 1,781.

Serikali tayari imetangaza kuzifungia Yanga na Simba kuutumia uwanja huo hadi hapo baadaye.

Mashabiki wa Simba waling’oa viti wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga kwenye uwanja huo, jana.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametangaza uamuzi huo na kusisitiza lazima gharama zilipwe.

Nape alifika katika eneo la uwanja huo na kukagua hali ilivyo baada ya uharibifu huo.

Tambwe alishika mpira kabla ya kuifungia Yanga, alipokwenda upande wa mashabiki wa Simba, tafrani kubwa likazuka na mashabiki hao wakaanza kuvunja viti.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV