October 2, 2016


Serikali inatoa tamko leo kuhusiana na uharibu wa viti zaidi ya 200 uliojitoteza jana kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Simba, waling'oa viti na kuvirusha uwanjani baada ya Amissi Tambwe kuifungia Yanga bao.

Kabla ya kufunga, Tambwe aliunawa mpira. Jambo hilo lilionekana kuwaudhi mashabiki hao ambao walianza kung'oa viti na kuvitupa uwanjani.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye atazungumza leo na waandishi wa habari.

Kwa hali ilivyo, kama si onyo lazima kutakuwa na adhabu ambayo hakika itakwenda kwa klabu ya Simba.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV