October 2, 2016


Mshambuliaji wa Simba, Shiza Kichuya alishindwa kujizuia na kumwaga chozi mara tu baada ya mechi kwisha.

Mechi ya watani, Yanga dhidi ya Simba iliisha kwa sare ya bao 1-1 baada ya Kichuya kuisawazishia Simba katika dakika ya 87 kwa mpira wa kona uliojaa moja kwa moja wavuni.
Lakini baada ya mechi, Meneja wa Simba, Mussa Hassan Mgosi alilazimika kufanya kazi ya ziada kumtuliza Kichuya.


Kichuya alionekana akimwaga chozi bila ya kueleza tatizo ni nini, ilikuwa furaha ya bao lake au machungu ya kubanwa na mwamuzi Martin Saanya kama ambavyo wachezaji wa Simba walivyokuwa wakilalamika.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV