November 27, 2016


Arsenal imeendeleza ushindi katika Ligi Kuu England kwa kuichapa AFC Bournemouth kwa mabao 3-1 kwenye Uwanja wa Emirates jijini London, leo.

Mabao ya Arsenal katika mechi hiyo, shukurani ziwaendee Alexis Sanchez aliyefunga mawili, bao la kwanza katika dakika ya 12, la tatu katika dakika ya 90 huku Theo Walcott akifunga la pili katika dakika ya 53.

Bournemouth walionyesha soka safi na la kuvutia lakini Arsenal walionekana kuwa na mpangilio mzuri tokea mwanzo. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV