November 27, 2016

GIDABUDAY (KULIA)

Chama cha Riadha Tanzania (RT), jana Jumapili kilifanya uchaguzi wake mkuu na kuwapata viongozi wapya watakaokiongoza chama hicho kwa miaka minne ijayo.

Katika uchaguzi huo uliofanyika kwenye Ukumbi wa Uwanja wa Taifa, Dar, Anthony Mtaka alichaguliwa kuwa rais, William Kalaghe (Makamu wa Rais - Utawala), Dk Ahmed Ndee (Makamu wa Rais - Ufundi), Wilhelm Gidabuday (Katibu Mkuu), Ombeni Zavala (Katibu Mkuu Msaidizi) na Gabriel Liginyani (Mweka Hazina).

Waliochaguliwa kuwa Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ni Lwiza Msyani, Meta Bare, Rehema Killo, Dk Nassor Matuzya, Robert Kalyahe, Zakaria Buru, Mwinga Sote, Tullo Chambo, Christian Matumbo na Yohana Mesese.

Akizungumza baada ya uchaguzi huo, Mtaka alisema atahakikisha anaanza kazi mara moja kuhakikisha mchezo wa riadha unapiga hatua kubwa kutoka hapo ulipo kufika anga za juu zaidi.
“Nitahakikisha nashirikiana na wajumbe wenzangu kuufanya mchezo huu kufika levo za juu,” alisema Mtaka.


0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV