November 24, 2016

LWANDAMINA (KUSHOTO) AKIWA NA MMILIKI WA BLOG YA SALEHJEMBE, SALEH ALLY.

Uongozi wa Yanga sasa umepanga kumtangaza Kocha wake mpya George Lwandamina.

Lwandamina raia wa Zambia, anatarajia kutambulishwa kesho kwenye makao makuu ya Yanga.

Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Clement Sanga imeelezwa ndiye atakayefanya zoezi hilo kesho.

Lwandamina amechukua nafasi ya Hans van der Pluijm ambaye sasa anakuwa Mkurugenzi wa Ufundi wa Yanga.


Awali, Yanga ilikataa kuwa kocha huyo yuko nchini hadi alipofichuliwa na SALEHJEMBE na kufanyiwa mahojiano.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV