November 22, 2016


Kocha wa Yanga, Hans van der Pluijm ambaye sasa amepata cheo na kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, amefungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi tatu.

Pluijm amefungiwa baada ya Kamati ya Saa 72 ya TFF kukaa na kubaini ana makosa.

Pluijm amfungiwa kukaa kwenye benchi kwa mechi tatu na kama hiyo haitoshi amepigwa faini ya mkwanja Sh 500,000.

Habari za ndani kutoka kwenye kamati hiyo zimeeleza kwamba kocha huyo Mholanzi alitoa maneno machafu kwa waamuzi wakati wa mapumziko katika mechi moja ya ligi kuu.

Pia akaendelea kufanya hivyo baada ya mechi kwisha alipowafuata vyumbani na kuwavurumishia maneno mengine. 


Adhabu hiyo inaonyesha itakuwa imetolewa kupitia kanuni 40 (1) ya Ligi Kuu Bara.

0 COMMENTS:

Post a Comment

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV